Kila Mtu ana Upungufu

Kila Mtu ana Upungufu

Mkwewe Musa akamwambia, jambo hili ufanyalo si jema. Huna budi utadhoofika wewe, na hawa watu walio pamoja nawe pia; maana jambo hili ni zito mno kwako; huwezi wewe kulitenda peke yako. —KUTOKA 18:17–18

Mungu alimtumia mkwewe Musa kumwambia Musa kwamba alikuwa akijaribu kufanya mengi. Huu ni ujumbe ambao Mungu ananena kwa wengi katika mwili wa Kristo leo. Wakati mwingine tunapenda kufikiri tuna nguvu nyingi. Hatupendi mtu kutuambia kwamba kitu ni kikubwa sana kwetu sisi kukabiliana nacho, na tunakisukuma na kukisukuma bila kujali tunavyohisi.

Wakati wote nilikuwa aina ya mtu aliyefikiri kwamba angeweza kufanya chochote nichodhamiria kufanya. Nilikuwa nina hakika kabisa kwamba ningetimiza kazi iliyokuwa mbele yangu. Mtu angeniambia kinyume, ilinifanya tu niamue kuwonyesha kwamba walikosea. Niligundua kuwa tukiwa na nia ya kuwa na lazima ya kufanya kila kitu, bila kujali kilivyo kigumu, tunaweza kujidhuru. Hatuwezi kujisukuma nje ya mipaka inayowezekana bila kushindwa.

Ukweli huu hapa: Mungu hatupatii nguvu za kitu chochote asichotuambia tufanye, lakini wakati wote hutupatia nguvu na uwezo wa kufanya kwa furaha na amani yote ambayo anatuongoza kufanya. Mungu anataka ufurahie maisha yako, na huwezi iwapo unaishi chini ya mfadhaiko usiokoma.


Je, kuna marekebisho yoyote unayohitaji kufanya ili kuwa mwenye afya, amani na katika kiasi?

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon