Kisiwe Kisingizio

Kisiwe Kisingizio

Bwana atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya. —KUTOKA 14:14

La kusikitisha ni kwamba, mara nyingi watu wengi huwa hawakubali ukweli ambao Mungu huwafunulia. Ni uchungu kukabili makosa yetu na kuyashughulikia. Tunaelekea kuthibitisha tabia mbaya. Huwa tunaruhusu mambo yaliyopita na jinsi tulivyolelewa kuathiri maisha yetu kwa njia hasi.

Huenda mambo yetu yaliyopita yakaeleza sababu za kuteseka kwetu lakini si lazima tuyatumie kama kisingizio cha kuishi katika utumwa.
Kila mtu hana cha kusingizia kwa sababu Yesu husimama tayari wakati wote kutimiza ahadi yake ya kutuweka huru. Yuko karibu nasi, na atatutembeza hadi kwenye msitari wa mwisho katika eneo lolote iwapo tutakuwa tayari kupitia kila jambo hadi mwisho naye.

Mungu huwa hatuachi na kutuacha bila usaidizi. Anatuahidi kwamba hataruhusu tujaribiwe kupita tuwezavyo lakini pamoja na lile jaribu, atafanya na mlango wa kutokea, ili tuweze kustahimili (1 Wakorintho 10:13).

Huenda ukawa na ngome kuu katika maisha yako ambazo zinahitaji kuvunjwa. Hebu nikuhimize kwa kusema, “Mungu yuko upande wako.” Katika vita vya kiroho vinavyoendelea katika mawazo yako, Mungu anapigania upande wako.


Haijalishi ukubwa wa majaribu yaliyo mbele zetu, Mungu ametuahidi kila kitu tunachohitaji ili kutembea katika ushindi.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon