Kiungo Muhimu Kinachokosekana

Kiungo Muhimu Kinachokosekana

Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba… —ZEKARIA 12:10

Ujumbe wa neema ya Mungu umekuwa ujumbe mmoja pekee muhimu sana ambao Roho Mtakatifu amenihubiria. Tajriba yangu yote ya Ukristo ilikuwa ya kung’ang’ana kabla nijifunze kuhusu nguvu za kiroho za neema. Kufundisha watu kuhusu imani na kukosa kuwafundisha kuhusu neema, kwa maoni yangu, ndiyo “kiungo muhimu kinachokosekana” katika safari ya watu wengi ya imani.

Neema ni nguvu za Roho Mtakatifu zilizopo ili kufanya kinachohitajiwa kufanywa katika maisha yetu, na nguvu za kuleta na kudumisha mabadiliko. Ni uwezo wa Mungu unaokuja kwetu bila malipo tukiuitisha. Kupitia kwa imani, neema ya Mungu inapokewa. Imani sio bei inayonunua baraka za Mungu, lakini ni mkono unaozipokea.

Kusikia tu neno neema ni kitulizo kwangu. Kumbuka kila wakati kwamba unapohisi kusikitika, ni kwa sababu umeingia katika nguvu zako mwenyewe na unahitaji kurudi katika nguvu za Mungu. Neema hukuacha ukiwa mwenye nguvu na mtulivu; kazi za mwili hukuacha ukiwa dhaifu, bila nguvu, ukiwa umesikitika na mwenye hasira. Mwegemee Mungu katika yote utakayofanya leo na kila siku, kwa sababu bila yeye, huwezi lolote (Yohana 15:5).


Pokea sio tu neema inayookoa, lakini pokea neema, neema, na neema zaidi ili uweze kuishi kwa ushindi na kumtukuza Yesu katika maisha yako ya kila siku.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon