Kuchagua Maneno Yako kwa Makini

Kuchagua Maneno Yako kwa Makini

Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu. MITHALI 17:28

Kitabu cha Mithali kimejaa Maandiko kuhusu kunyamaza kwa sababu kuna hekima katika utulivu. Wakati mwingine kitu cha hekima unachoweza kusema ni kutosema kitu kabisa. Kabla hujaanza kusema kuhusu vitu unavyohisi mvuto wa kusema, jiulize kweli unahitaji kusema mangapi kuvihusu. Nyamaza na usikize kile Mungu anasema. Hutawahi kujuta kusema kile ambacho anataka useme, vile yeye mwenyewe angekisema.

Ningependa nikuhimize kumanikia vitu chanya na ushukuru kwa vitu hivi. Vile Warumi 12:21 inasema, tunashinda mabaya kwa mema. Kwa maneno mengine, tukiwa katika shughuli za kutenda mema, hakutakuwa na nafasi ya mabaya. Kwa hivyo lifanye lengo lako kutenda yaliyo mema mbele ya Mungu, na ufurahie uhuru na ushindi yanayoleta katika maisha yako.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwamba ninaweza kuishi katika hekima unayonipa. Nisaidie kujua wakati wa kusema na wakati wa kunyamaza. Iwapo ni mazungumzo ambayo sifai kuchangia, ninakushukuru kwamba utanisaidia kujidhibiti na kuwa na nidhamu ya kutosha kufanya hivyo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon