Kuendelea kwa Kazi

Kuendelea kwa Kazi

. . . mlipopata lile neno la ujumbe la Mungu mlilosikia…na ndivyo lilivyo kwelikweli; litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini. —1WATHESALONIKE 2:13

Ninawahimiza kusema kila siku, “Mungu anatenda kazi ndani yangu sasa hivi—Ananibadilisha!” Sema kutoka kwa kinywa chako linavyosema Neno, sio vile unavyohisi. Tukisema tu kuhusu vile tunavyohisi peke yake, itakuwa vigumu Neno la Mungu kufanya kazi ndani yetu kwa mafanikio.

Tunapochukua hatua kila tunachoweza kuwa katika Kristo, tutafanya baadhi ya makosa—kila mtu hufanya. Lakini hutuondolea mshinikizo tunapotambua kuwa Mungu anatutarajia kufanya tu kadri tuwezavyo. Hatutarajii kuwa wakamilifu. Iwapo tungekuwa wakamilifu, tusingalihitaji mwokozi. Ninaamini kwamba wakati wote Mungu ataacha idadi fulani ya kasoro ndani yetu, ili tujue tu vile tunavyomhitaji Yesu kila siku. Mimi si mhubiri mkamilifu. Kuna nyakati ambazo huwa ninasema vitu kwa njia isiyo sahihi, nyakati ambazo huwa ninafikiri nimesikia kutoka kwa Mungu na kugundua kuwa nilikuwa nikisikia kutoka kwangu. Kuna nyakati nyingi ambazo huwa ninapungukiwa na ukamilifu. Sina imani kamilifu, fikra kamilifu, nia kamilifu na njia kamilifu.

Yesu alijua hayo yatafanyika kwetu sote. Ndiyo kwa sababu anasimama katika pengo kati ya ukamilifu wa Mungu na kasoro zetu. Anaendelea kutuombea kila mara kwa kuwa tunayahitaji maombi hayo (Waebrania 7:25).


Hatuna lazima ya kuamini kuwa Mungu hutukubali tu tunapotenda kikamilifu. Tunaweza kuamini ukweli kwamba anatukubali “ndani ya Mpendwa” (Waefeso 1:6).

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon