
Basi farijianeni na kujengana kila mtu na mwenzake, vile vile kama mnavyofanya. 1 WATHESALONIKE 5:11
Mojawapo ya vitu vizuri zaidi unavyoweza kumfanyia mtu ni kumhimiza na kumjenga. Mwambie mtu aliye karibu nawe kitu chanya kuhusu vile walivyo au vile unavyowafurahia. Au waambie vile Mungu anavyowapenda na anavyotaka kuwabariki. Himizo lina nguvu. Hufanya watu wahisi vizuri zaidi kwa kila njia.
Ninakumbuka wakati mmoja nilipopata ujumbe kutoka kwa mtoto wangu mdogo. Kile ujumbe huo ulisema ni “Ninakupenda, Mama!” Wakati huo nilihisi kuhuishwa na maneno yake. Yalinipa dozi zaidi ya nguvu nilizohitaji siku hiyo.
Fikiria kuhusu watu ambao utakaribiana nao leo. Shukuru kwamba wako maishani mwako, na umwombe Mungu akusaidie kuwanenea maneno ya himizo. Huenda ukashangaa tofauti yatakayoleta, sio tu kwao peke yao bali kwako pia.
Sala ya Shukrani
Baba, ninapoendelea na shughuli zangu za siku, ninaomba unionyeshe njia za kuwahimiza na kuwajenga watu. Asante kwa nafasi unazonipa kuleta tofauti katika maisha ya wengine. Ninataka kukamata nafasi zangu leo.