Kuishi Huru Bila Mizigo

Kuishi Huru Bila Mizigo

Uzito katika moyo wa mtu huuinamisha; bali Neno jema huufurahisha. MITHALI 12:25

Katika maisha haya, kila wakati tutakuwa na nafasi ya kufadhaika, kuwa na wasiwasi na kuhangaika. Shetani atahakikisha hilo kwa sababu anajua kwamba mfadhaiko hutuinamisha. Shetani anapojaribu kuleta mfadhaiko ndani ya mioyo yetu, tunaweza kumpa Bwana mfadhaiko huo katika maombi kwa shukrani, huku tukifanya matakwa yetu yajulikane naye. Tukapofanya hivyo tutapata amani ya kuishi huru bila mizigo.

Ninakuhimiza kukataa kuinamishwa na wasiwasi. Badala yake, mgeukie Bwana katika maombi, ukifurahia katikati ya kila hali. Mungu ni mwaminifu, na atapeana amani na furaha ambayo ameahidi kwa wale wote wanaokataa kukubali wasiwasi na hofu na badala yake kumgeukia kwa imani rahisi na tumaini.


Sala ya Shukrani

Baba, ninapoanza kuwa na hisia za wasiwasi au mfadhaiko, nisaidie kukupa mizigo hiyo. Asante kwamba sihitaji kuishi zaidi chini ya mizigo mizito. Asante kwa kuwa ninaweza kuleta wasiwasi wangu kwako ili niweze kuishi maisha ya amani.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon