Kujiamini kupitia Kristo

Kujiamini kupitia Kristo

Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili. Wafilipi 3:3

Kujiamini kwa kweli kamwe hakutokani kwa jinsi tunavyohisi au tunachoweza au hatuwezi kufanya – inatoka kwa kuwa na ufunuo wa sisi ni nani ndani ya Kristo. Wakati tunajua kwa kiasi gani Mungu anatupenda na tunapokea uponyaji wake kutokana na maumivu ya zamani, basi hatuhisi tena haja ya kuimarisha ujasiri wetu juu ya mambo ya mwili.

Naweza kukumbuka miaka mingi iliyopita wakati nilijitahidi na kukosa ujasiri kwa sababu sikuwa na shahada ya chuo kama wahubiri wengine niliowajua. Nashukuru kwa sababu wakati  nilianza kuzingatia upendo wa Mungu usio na masharti kwangu, nilijifunza kuanzisha imani yangu juu ya kile ambacho Neno lake linasema juu yangu-haki ya Mungu katika Kristo Yesu (tazama 2 Wakorintho 5:21).

Yesu anataka kurejesha uaminifu wa kweli katika maisha yako kwa kukuponya kutoka kwa mambo yaliyopita ambayo yameathiri jinsi unayojitazama mwenyewe. Unapoangalia kile kilicho sawa na Mungu badala ya kile kilicho kibaya na wewe, utaanza kutembea katika ujasiri unaotokana na kuwa ndani Yake.

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, nisaidie kuelewa mimi ni nani ndani ya Kristo na kupokea uponyaji wako katika mawazo na hisia zangu. Ninaamua kuweka imani yangu ndani yako!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon