Kujinasua

Hakuna apigaye vita ajitiaye katika shughuli za dunia, ili ampendeze yeye aliyemwandika awe askari. —2 TIMOTHEO 2:4

Ushawahi kujipata ukikosa muda wa kuwa na Mungu kwa sababu unashughulikia mambo mengine? Katika 2 Timotheo 2:4, Paulo anamwambia mwanafunzi wake Timotheo, kwamba askari mwenye hekima hujiepusha kuingia katika vitu ambavyo havitampendeza mtu aliyemwajiri. Kwa maneno mengine, mwana wa Mungu anayetaka kumpendeza Mungu hulenga kufanya yaliyo muhimu na kujiepusha na vitu ambavyo vitamwondoa kwa yaliyo muhimu.

Ili kumkaribia Mungu kila siku, itabidi ujiepushe na vitu visivyo muhimu, pamoja na mitego ya ulimwengu. Huenda hili likamaanisha, kusema la kwa jambo ambalo ungependa kufanya lakini huna nafasi ya kulifanya kabisa. Inaweza kumaanisha kuwa na mipaka mizuri na sio kujiingiza sana katika matatizo ya watu. Ni muhimu kusaidia watu, lakini kuna tofauti kati ya uhusikaji wa kiungu na kuwa katika mtego wa kusaidia. Huenda hata ikamaanisha kukosa kufikiri kuhusu mifadhaiko na mizigo ya maisha inayotokea katika siku, kwa kuwa bila shaka zinaweza kutuondoa kwenye mapenzi ya Mungu na kusudi juu ya maisha yetu.

Mungu anakupenda na anataka kuwa katika uhusiano nawe. Usiache mitego ya ulimwengu ikuzuie kufurahia ushirika wa kila siku naye.


Usiache vitu visivyo muhimu kuchukua nafasi ya kwanza kuliko vitu muhimu katika maisha yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon