Kujitokeza Kufanya Vitu Vipy

Kujitokeza Kufanya Vitu Vipy

Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu; bali wenye haki ni wajasiri kama simba. MITHALI 28:1

Mungu alikuumba kwa ajili ya maisha ya furaha ambayo yanakuhitaji kuchukua hatua za ujasiri za imani, halafu umwone akikutendea. Watu wengi hawajaridhishwa na maisha yao tu kwa sababu hawajitokezi kufanya vitu vipya ambavyo wanatamani kuwa navyo. Wanataka kubaki katika “eneo salama,” ambalo unahisi salama, lakini mara nyingi sio eneo ambalo furaha na msisimko wa maisha unaweza kupatikana.

Tunaweza kushukuru kwamba Mungu ana maisha ya kusisimua kwa ajili yetu. Usiache hofu ikuzuie kufurahia maisha hayo na kuharibu hatma yako. Vile ninavyopenda kusema, “Hisi hofu hiyo na ufanye hata hivyo—fanya kwa hofu!”

Ninakuhimiza kujumlisha mambo tofauti tofauti katika maisha yako. Jaribu vitu vipya; ukianza kuhisi kwamba maisha yameanza kukosa ladha na kupata uozo, ongeza ladha kidogo kwa kufanya kitu tofauti. Anza kufikiri na kusema, “Sitaishi katika hofu.”


Sala ya Shukrani

Baba, ninaomba kuwa utanisaidia kutoka kwa haya maisha ya kuchosha, yasiyo ya kusisimua na ya kawaida. Ninakushukuru kuwa una maisha ya kusisimua na yenye furaha kwa ajili yangu. Na ninashukuru kwa matukio mapya yatakayotokea hivi karibuni. Nisaidie kufurahia kila kitu kipya utakachoniletea.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon