Kukabiliana na ukweli huleta maisha ya furaha

Kukabiliana na ukweli huleta maisha ya furaha

Ijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa. 2 Wakorintho 13:5

Hakuna mtu anayeweza kuachiliwa kutokana na tatizo mpaka awe tayari kukubali kuwa na tatizo. Mnywaji wa pombe, madawa ya kulevya au mtu yeyote ambaye amepoteza udhibiti wa maisha yake atadhoofika mpaka aweze kusema, “Nina tatizo na ninahitaji msaada.”

Ingawa matatizo yetu huenda yaliletwa kwa sababu ya kitu kilichofanyika kinyume na mapenzi yetu, hatufai kuruhusu tatizo hilo kuendelea, kukua na kuchukua udhibiti juu ya maisha yetu yote. Maisha yetu ya zamani yanaweza kutufikisha tulipo, lakini hatupaswi kukaa kwa njia hiyo. Tunaweza kuchukua hatua kwa kuchukua hatua nzuri za kubadili mambo-na tunaweza kufanya kwa msaada mwingi kutoka kwa Roho Mtakatifu.

Haijalishi kile shida yako inaweza kuwa, unapaswa kukabiliana na ukweli na kuchukua dhima fulani ya kibinafsi. Biblia inasema tunapaswa kujitathmini wenyewe. Hiyo inaweza kuonekana kuwa ya kutisha, lakini Yesu Kristo yuko ndani yako na anaweza kukusaidia kupitia shida na masuala yoyote ya zamani.

Kabiliana na ukweli-inaweza kuwa mwanzo wa maisha ya furaha zaidi!

OMBI LA KUANZA SIKU

Roho Mtakatifu, sitaki kuishi katika kukataa na hofu ya matatizo yangu. Ninaamua kujitathmini na kufikia chini ya masuala haya kwa sababu najua Unaweza kunisaidia kufanyiza kazi ili niwe na furaha zaidi.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon