Kukataa Tamaa sio Suluhu

…Tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu… — WAEBRANIA 12:2

Haichukui talanta yoyote maalum mtu kukata tamaa na kulala kando ya barabara ya maisha na kusema, “Nilikata tamaa.” Mtu yeyote hata kama ni aaminiye au la, anaweza kufanya hivyo.

Kukata tamaa ni majaribu yanayotukabili wakati mmoja au mwingine, lakini ukimkaribia Yesu, au vyema zaidi akikukaribia, anaanza kupuliza nguvu, nishati na ujasiri ndani yako. Na kitu cha ajabu kinaanza kutendeka—anakufanya utake kuchuchumilia mbele!

Nilikuwa na mazoea ya kutaka kukata tamaa na kuondoka. Lakini sasa ninaamka na kuanza kila siku upya. Ninaanza siku yangu kwa kuomba, kusoma Biblia na kusema Neno, nikimtafuta Mungu. Ni jambo la kushangaza tofauti inayotokea unapoanza siku yako kwa kumkaribia Mungu.

Unapohisi hamu au majaribu ya kukata tamaa, usikubali. Mtazame Yesu na uufuate mfano wake. Alichuchumilia mbele hata katika hali ngumu sana, na atakupatia nguvu za kufanya vivyo hivyo. Ni Kiongozi wako; Yeye ni Chanzo na Mtimizaji wa imani yako.


Hebu tufanye uamuzi leo kwamba, hata lije lipi, tutaendelea kuchuchumilia mbele, tukimtazama Yesu, bila kujali.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon