kumwamini Mungu kupitia majaribio ya kihisia

kumwamini Mungu kupitia majaribio ya kihisia

akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. Luka 22:42

Kukua Mkristo aliye komaa ambaye anamfuata Roho Mtakatifu sio jambo linalofanyika usiku mmoja-ni mchakato wa kujifunza ambao unachukua muda. Pole pole, uzoefu mmoja baada ya mwingine, Mungu hujaribu na kupima hisia zetu, kutupa fursa za kukua.

Mungu anatuwezesha kukabiliana na hali ngumu ambazo huchochea hisia zetu. Kwa njia hii, wewe na mimi tunaweza kujisikia wenyewe jinsi hisia zinaweza kutulemea na jinsi tunahitaji sana msaada wake.

Yesu alionyesha mfano huu kwa ajili yetu. Usiku kabla ya kufa kwa ajili ya dhambi zetu, alikuwa na shida kubwa ya kihisia. Yeye hakutaka kufa, lakini alizipita hisia zake na akamwomba Mungu, “Sio mapenzi yangu, bali yako yatimizwe.” Mambo hakika hayakuwa mazuri mara moja, lakini hatimaye Yesu alitokea kwa ushindi na kupita hali hiyo.

Unaweza kufanya hivyo kupitia majaribio yako ya kihisia. Yesu hakuongozwa na hisia zake, na huhitaji kuwa hivyo. Wakati mambo yanakuathiri kihisia, chukua nafasi hiyo na uione kama fursa ya kuingia mahali pa kumtegemea Mungu kabisa.

OMBI LA KUANZA SIKU

Bwana, najua kwamba ninaweza kukuamini wakati majaribio ya kihisia yanakuja. Pamoja na Yesu kama mfano wangu, nasema, “Sio mapenzi yangu, lakini mapenzi yako yafanyike.” Unajua kilicho bora kwangu na ninakuamini kabisa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon