kujifunza kusema “sio biashara yangu”

kujifunza kusema "sio biashara yangu"

Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. Mathayo 7:1

 Maelfu ya mambo tunayokutana nayo kila siku si ukweli wala si uongo lakini ni uchaguzi wa kibinafsi-uchaguzi ambao watu wana haki ya kufanya wenyewe bila kushurutishwa.

Ibilisi hushughulika sana kuwapa mapepo kazi ya kutupa mawazo ya kuhukumu, na mawazo muhimu katika akili za watu. Ninaweza kukumbuka wakati nilkuwa nafurahi kukaa katika hifadhi au maduka ya ununuzi na kuangalia watu wote wakipita nami nilifanya maoni akilini juu ya kila mmoja wao-mavazi yao, mitindo, marafiki na kadhalika.

Lakini Biblia inasema ni makosa kuwahukumu watu kwa njia hii. Hatuwezi kamwe kujizuia kuwa na maoni, na hakuna kitu kibaya na hilo, lakini wakati tunadhani kuna kitu kibaya na watu wengine kwa sababu hawashiriki mapendekezo yetu binafsi, tuna tatizo la kuhukumu wengine.

Katika hali hizi, mimi hujiambia mwenyewe, Joyce, sio biashara yako. Usiruhusu hukumu za hatari zikue ndani yako. Badala yake, kumbuka kwamba Mungu alifanya kila mtu tofauti na ni sawa kwa watu kufikiri tofauti. Na wakati wa lazima, jiambie mwenyewe, hii sio biashara yangu.

 OMBI LA KUANZA SIKU

 Mungu, sitaki kuhukumu au kulaumu wengine. Ninapokutana na watu ambao wana maoni tofauti na mapendekezo ya kibinafsi kuliko mimi, tafadhali nisaidie kuwaona kupitia macho yako na kukumbuka kuwa maoni yangu si muhimu zaidi kuliko yao.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon