Kuongozwa na Roho

Tukiishi kwa Roho na tuenende kwa Roho (Wagalatia 5:25)

Andiko la leo linazungumza kuhusu kuishi na kutembea kwa Roho, ambayo ni sawa na kuongozwa na Roho. Kuna vitu vingi vilivyopo vya kutuongoza – watu, shetani, mwili (miili yetu, nia, hiari na hisia), au Roho Mtakatifu. Kuna sauti nyingi ulimwenguni zinazotuzungumzia, na kwa wakati mmoja. Ni muhimu kwetu sisi kujifunza kuongozwa na Roho Mtakatifu. Kumbuka: Ni yeye anayejua mapenzi ya Mungu na aliyetumwa kukaa ndani ya kila mmoja wetu ili kutusaidia kuwa kile Mungu alitupangia kuwa na kuwa na kila kitu ambacho anataka tuwe nacho.

Roho Mtakatifu anaishi ndani yetu ili kutusaidia. Huenda usaidizi wake usifurahiwe mara ya kwanza, lakini shukuru Mungu kwamba ni wa kushikilia na hawezi kusalimu amri kwa ajili yetu. Tunafaa kuinua maisha yetu yote kila siku na kusema Roho Mtakatifu, umekaribishwa katika kila eneo la maisha yangu!”

Unapomkaribisha Roho Mtakatifu katika kila eneo la maisha yako atakuja. Atazungumza nawe, akuelekeze, akurekebishe, akusaidie, akuwezeshe, na kukuongoza. Nguvu zingine zinaweza kujaribu kukuongoza, lakini Roho Mtakatifu hukupa nguvu za kuzipinga na kukuwezesha kumfuata.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Jiulize anayeongoza maisha yako. Ni wewe, watu wengine, hisia, uongo wa shetani, au Roho Mtakatifu?  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon