Kupokea Urithi

Kupokea Urithi

Na kama tu watoto, basi, tu warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate kutukuzwa pamoja naye. WARUMI 8:17

Mtazamo wetu kuhusu Mungu, sisi wenyewe, na mpango wake kwa ajili yetu ni mdogo sana. Mungu anataka tutoke nje ya udogo na kuona ukubwa wa mwito wake na urithi wetu ndani yake. Tunaporithi kitu, ina maana kuwa tunapata kitu ambacho mtu mwingine alifanyia kazi. Yesu alipata thawabu kwa ajili yetu. Alifanya kazi na kupata tunachorithi, na kile tunachoweza kufanya ni kushukuru na kukipokea kwa imani. Hakuna kitu kingine kinachohitajika.

Hatua moja ya Imani ni—kuamini tu na kupokea wema wa Mungu—hili litakuweka katikati ya urithi mkuu ambao uliwahi kupitishwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Hiyo hatua ya imani huondoa kung’ang’ana na fadhaa maishani. Kama 1 Yohana 4:17 inavyosema “vile alivyo, ndivyo tulivyo ulimwenguni humu.” Hizo ni habari njema za kushukuru kwazo!


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwamba mimi ni mwanao. Asante kwa kila kipawa na kila upaji ambao umeahidi. Na asante kwamba nina urithi wa maisha ya milele nawe kwa sababu ya kazi ya Yesu kwa niaba yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon