…Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake. MATHAYO 12:34
Kadri tunavyohimiza watu, ndivyo wanavyoshawishika vizuri zaidi. Kwa kweli, sifa husaidia watu kufanya mambo vizuri zaidi, huku manung’uniko yakiwafanya kufanya mambo vibaya zaidi.
Chagua mtu ambaye ungependa kuwa na uhusiano naye na uanze kumsifu kwa ukweli na kwa bidii. Ninaamini utashangaa vile watakavyofanya mambo vizuri zaidi baada ya sifa hizo. Huenda wasiwasi yako ya kwanza ikawa, nikipuuza makosa yao, si watanidharau? Bila shaka hilo linaweza kufanyika, lakini mara nyingi huwa halifanyiki.
Mara nyingi kile hufanyika ni kwamba mtu anayehimizwa huwa anashukuru sana kwa himizo, mtu huyo huwa na mabadiliko ya moyo. Hatimaye huwa wanatia bidii zaidi kwa upande wao ili kuboresha uhusiano huo. Sasa hufanya hivyo kwa hiari yao na sio kwa sababu unajaribu kuwalazimisha.
Sala ya Shukrani
Asante, Baba, kwamba unanihimiza na kunijenga kupitia kwa ahadi zilizo katika Neno lako. Ninaomba kwamba utanisaidia kuwafanyia wengine hayo hayo. Asante kwa kunionyesha njia za kuhimiza watu walio katika maisha yangu leo.