Kushinda

Kushinda

Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu; bali wenye haki ni wajasiri kama simba. —MITHALI 28:1

Woga huibia watu imani yao. Hofu ya kushindwa, hofu ya binadamu, na hofu ya kukataliwa ni baadhi ya hofu kubwa zinazotumiwa na shetani ili kutuzuia kuendelea.

Lakini hata adui akituma hofu ya aina gani dhidi yetu, kitu cha muhimu ni kushinda. Tunapokabiliwa na hofu, hatufai kuacha itushinde. Ni muhimu kwa ushindi wetu tukiamua kwamba, “Kwa usaidizi wa Mungu, nitashinda.”

Mwitiko wa kawaida kwa hofu ni kutoroka. Adui anataka tutoroke; Mungu anataka tusimame kwa utulivu na tuone ukombozi wake. Kwa sababu ya hofu watu wengi hawakabiliani matatizo; hutumia muda wao wakitoroka kila mara. Tunafaa kujifunza kusimama kwa uthabiti na kukabili hofu, tukiwa salama kwa kujua kwamba sisi ni zaidi ya washindi ndani ya Kristo (Warumi 8:37).

Hofu ya kushindwa hutesa wengi. Tunaogopa vile watu watafikiria kutuhusu tukishindwa. Tukichukua hatua halafu tushindwe watu wengine watasikia kuhusu hilo; lakini huwa wanasahau haraka kuhusu hilo tukilisahau na kuendelea. Ni bora kujaribu kitu na kushindwa kuliko kukosa kujaribu kitu na kufaulu.


Kabili maisha kwa ujasiri. Roho wa Mungu yuko ndani yako—kwa hivyo amua kutoogopa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon