Kusikiliza Mungu Anaponena

Kusikiliza Mungu Anaponena

Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata. YOHANA 10:27

Ni muhimu tusifikirie eti tunapofanya maombi na kuwa na ushirika na Mungu ni sisi tu tunaoongea wakati wote. Tunaweza pia kutenga muda na kukaa naye tukisikiliza tu. Maombi ni sarafu ya pande mbili. Mungu huwa hatusikizi tu, shukuru kwamba anaongea nasi pia.

Zoezi kuu la kufanya unapomsikiza Mungu ni kumuuliza iwapo kuna mtu angetaka uhimize au ubariki—halafu utulie na kusikiza. Utashangaa jinsi atakavyojibu haraka. Ataujaza moyo wako fikra na malengo ya kiungu. Bila kutarajia watu wengine watakujia mawazoni na mawazo ya kiubunifu kuhusu vile utakavyowabariki na kuwahimiza. Haya “mawazo” na “”fikra” ni Mungu akiongea nawe. Mungu huongea kwa njia nyingi tofauti, lakini kitu kimoja ni cha hakika: Tutaikosa sauti yake tusipojifunza kusikiza.

Mungu ana mawazo ambayo hujafikiria ambayo anataka kuwasilisha kwako. Msikize kwa makini na moyo uliyojaa shukrani kwa sababu ya uwepo wake. Halafu ufuate ushauri uliotolewa katika Yohana 2:5—“Lolote atakalowaambia, fanyeni.”


Sala ya Shukrani

Baba, ninakushukuru kwamba bado unaongea na watu wako. Ninaomba kwamba utanionyesha mtu ambaye anahitaji kuhimizwa leo. Asante kwa kuongea nami na kuniruhusu kuwa baraka katika maisha ya mtu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon