Kuumbwa na Kusudi

Kuumbwa na Kusudi

“Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.” YEREMIA 29:11 BIBLIA

Kama watoto wa Mungu, mojawapo ya vitu ambavyo tunaweza kushukuru kwavyo ni ufahamu kwamba Mungu ametukusudia kufanya mambo makubwa. Alikuumba kwa kusudi. Ana nafasi nyingi za kufanya mambo anazotaka kukupa na kazi anazotaka kuweka amana kwako.

Nina hakika umetambua kwa hiyo hoja kwamba utakabiliwa na pingamizi katika maisha yako unapomfuata Mungu. Watu walioitiwa ukuu, hukutana na changamoto kuu. Mungu hakutuahidi kwamba itakuwa rahisi. Kwa kweli, anatuhakikishia kuwa tutakuwa na dhiki katika ulimwengu (tazama Yohana 16:33). Lakini anaahidi pia kuwa nasi katika shida, kupigana kwa niaba yetu, na kututia nguvu za kushinda kizuizi chochote kinachotukabili.

Hata kitu gani kikizuia, endelea kumfuata Bwana kwa imani na kwa moyo wenye shukrani, ukijua kuwa amekukusudia kufanya mambo makuu kwa utukufu wake.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru, Mungu, kwamba umenipa tumaini na mustakabali. Nisaidie kufuata mwongozo wako na kutembea katika hatma yangu. Ninaamini uongozi wako, na ninashukuru kwa ajili ya uwepo na nguvu zako katika maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon