Kuwa Aaminiye Anayeamini

Kuwa Aaminiye Anayeamini

Kwa hiyo, kama anenavyo Roho Mtakatifu, leo, kama mtaisikia sauti yake, msifanye migumu mioyo yenu. Kama wakati wa kukasirisha, siku ya kujaribiwa katika jangwa. — WAEBRANIA 3:7– 8

Katika Waebrania, tunaona hali mbaya mbili za moyo—moyo mgumu na moyo usioamini. Katika jangwa, moyo mgumu uliwafanya Waisraeli waasi. Mtu wa moyo mgumu hawezi kumwamini Mungu upesi, ambayo ni shida kubwa kwa sababu kila tunachopokea kutoka kwa Mungu huja kupitia kwa kuamini. Ili kupokea kutoka kwake, kile tunachofaa kufanya ni kuja kwake katika imani ya upesi kama ya mtoto na kuamini tu.

Tunajiita waaminio, lakini ukweli ni kwamba, kuna “waaminio wasioamini” wengi. Kwa muda mrefu, nilikuwa mmoja wao. Nilikuwa nimedhuriwa sana utotoni mwangu, nikawa na ugumu wa moyo ambao Mungu alilazimika kuvunja katika maisha yangu.

Hata Musa alifika mahali ambapo katika jangwa ambapo hakuwa na upesi wa moyo kuamini Mungu. Ndiyo kwa sababu ni muhimu kwetu kuwa macho kiroho ili tuwe wepesi wa kuamini na kutembea katika imani siku hata baada ya nyingine. Tunaweza kuchagua kutahadhari kwenda kutoka imani hata nyingine na sio kuanza kujichanganya katika shaka yoyote au kutokuamini. Moyo unaoamini ni muhimu iwapo tunataka kuishi katika uhusiano wa karibu na Mungu.

Yesu anataka kurejesha nafsi yako, hata hisia. Mruhusu Yesu kuingia katika hayo maeneo ya maisha yako ambayo mtu mwingine yeyote hataweza kuingia. Muombe akubadilishe uwe mtu aliye na moyo kama alio nao.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon