Kuwa na Nia Chany

Kuwa na Nia Chany

Tumezitafakari fadhili zako, Ee Mungu, katikati ya hekalu lako. ZABURI 48:9

Nia chanya—nia zilizojaa imani na matumaini—huzalisha maisha chanya. Nia hasi—nia zilizojaa woga—huzalisha maisha hasi. Katika Mathayo 8:13, Yesu anatuambia kwamba tutafanyiwa vile tumeamini. Hii haina maana kuwa mimi na wewe tunaweza kupata kitu chochote tunachotaka kwa kukifikiria tu. Mungu ana mpango mtimilifu kwa kila mmoja wetu, na hatuwezi kumdhibiti kwa mawazo na maneno, lakini tukitaka mpango wake, tunafaa kuongea na kuwaza kulingana na mapenzi na mpango wake juu yetu.

Ninakuhimiza kufikiria kwa uchanya kuhusu maisha yako na kushukuru kwa sababu ya vitu vizuri ambavyo Mungu anafanya na atakavyovifanya. Jizoeshe kuwa na fikra chanya katika kila hali inayotokea; hata kama unapitia hali ngumu, simama kwa imani, ukiamini Mungu ataleta mema kutokana nayo vile ameahidi katika Neno lake.


Sala ya Shukrani

Baba, nisaidie kuyaelekeza maneno na mawazo yangu kwako wewe. Ninakushukuru kuwa umehifadhi vitu vizuri kwa ajili ya maisha yangu. Ninakuamini leo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon