Kuzungumza na Kusikiliza

Uisikie sauti ya kilio changu, Ee Mfalme wangu na Mungu wangu (ZABURI 5:2)

Maombi ni rahisi tu sana; si kitu zaidi ya kuzungumza na Mungu na kusikiliza kile anachosema. Mungu anataka kufundisha kila moja wetu kuomba na kusikia sauti yake kwa njia za kibinafsi. Anataka tu kutuchukua tulivyo na kutusaidia kugundua rithimu yetu ya kipekee ya maombi na kuanzisha mtindo wa maombi ambao unazidisha uhusiano wetu wa kibinafsi naye. Anataka maombi yawe njia rahisi, ya kawaida  na mawasiliano yanayotoa uhai tunapompa mioyo yetu na kumruhusu kutupatia moyo wake.

Mungu ni mbunifu sana kiasi cha kufundisha kila mmoja wetu kuingiliana naye kwa maombi kwa njia zinazotofautiana. Ni yeye alituumba kwa njia tofauti na hufurahia utofauti wetu. Sisi wote tuko mahali tofauti katika kutembea naye, tuko katika viwango tofauti vya ukomavu wa kiroho, na tuna tajriba tofauti na Mungu. Tunapokuwa katika uwezo wetu wa kuzungumza na Mungu na kusikiliza sauti yake, tunahitaji kumwambia Mungu kila mara, “Nifundishe kuomba; nifundishe kuzungumza nawe na kukusikiliza kwa njia ambazo ni nzuri sana kwangu. Nifundishe kusikia sauti yako kwa kiwango cha kibinafsi. Mungu, ninakutegemea wewe kunifanya niwe na athari katika maombi na kufanya uhusiano wangu nawe kupitia kwa maombi uwe wenye utajiri na kipengele kinachotuza sana cha maisha yangu.”

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Wewe ni kiumbe cha kipekee cha Mungu. Sherehekea hilo katika maisha yako na katika maombi yako.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon