Maombi ya Wakati Wowote, Mahali Popote

Maombi ya Wakati Wowote, Mahali Popote

Ee nafsi, umhimidi Bwana. Naam, vyote vilivyo ndani yangu vilihimidi jina lake takatifu! ZABURI 103:1

Kuomba mchana kutwa huku tukiendelea na shughuli zetu ni muhimu kama vile kutenga muda ili kuomba. Ninaamini Mungu anataka tumtambue, tufanye sala za maombi, na kutoa shukrani mchana kutwa kila siku. Jifunze kuacha maombi yawe jambo la kawaida kama kupumua.

Hebu fikiria vile utakavyohisi iwapo watoto wako watasema, “Ninakupenda, Mama” au Ninakupenda, Baba!” kila mara wanapotembea karibu nawe. Mmojawapo wa wanangu akipitia nyumbani kwangu ama ofisini na aseme, “Hujambo, Mama wewe ni mzuri! Nimekuja kukwambia tu hilo,” hilo hufanya siku yangu iwe nzuri.

Kujuza watu kwamba unafikiri ni wazuri, ni aina ya mawasiliano ambayo hukuza uhusiano. Tukimfanyia Mungu hivyo, uhusiano wetu naye utakuwa wa ndani na kuimarika, na tutaunganika naye kupitia kwa maombi ya “wakati wowote, mahali popote.” Na anapenda hivyo.


Sala ya Shukrani

Ninakupenda Baba, na ninashukuru kwamba unanipenda pia. Ninataka kuchukua kila nafasi kukwambia ulivyo wa ajabu na vile nilivyobarikiwa. Asante kwamba mimi huja kwako kwa maombi wakati wowote, mahali popote.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon