
Nalimngoja Bwana kwa subira, akaniinamia akakisikia kilio changu. Zaburi 40:1
Wakati mwingine hatutarajii chochote; tunangoja tu kusikia kitakachofanyika na hakuna kinachofanyika kwa sababu tumekuwa hatutarajii chochote. Wakati mwingine tunaweza kuanguka kwenye mtego wa kutarajia kusikitika kwa sababu tumesikitishwa mara nyingi hapo nyuma, kwa hivyo tunaogopa kutarajia chochote. Lakini Mungu anataka tuwe na matarajio ya wema wake yaliyojaa imani, kwa sababu anaweza kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo (tazama Waefeso 3:20).
Kuanza kuwa na nia ya shukrani kwa ajili ya wema uliopo wa Mungu katika maisha yako itafungua mlango kwa Mungu kufanya hata zaidi. Acha ajue kwamba unatarajia kuona wema wake katika maisha yako, sio kwa sababu unastahili lakini kwa kuwa yeye ni mwema!
Biblia inatufundisha kuwa Mungu anangoja kubariki watu, lakini anamtafuta mtu anayetarajia na kuamini kwa ajili ya huruma zake (tazama Isaya 30:18).
Sala ya Shukrani
Ninakushukuru leo, Baba, kwamba unaahidi katika Neno lako kwamba unanipenda na una mpango mkubwa juu ya maisha yangu. Ninashukuru kwa upaji wako mwingi, na ninasimama katika imani nikingoja wema wako kwa matarajio chanya.