Milango Wazi ya Uchungu

Milango Wazi ya Uchungu

Wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha. —ZABURI 126:5

Kwa wengi wetu, kusamehe mtu aliyetudhuru ndiyo sehemu ngumu sana ya uponyaji wa kihisia. Inaweza hata kuwa kikwazo kinachouzuia. Waliodhuriwa vibaya na wengine wanajua kwamba ni rahisi sana kusema neno nimekusamehe kuliko ilivyo kufanya.

Kwanza, acha niseme kwamba haiwezekani kuwa na afya nzuri ya kihisia huku ukiwa umebeba uchungu, chuki na kutosamehe mtu fulani. Ni sumu kwa mwili wako. Na ni vigumu kupata nafuu iwapo ipo.

Mwishowe nilimruhusu Bwana kuanza kazi kufanya kazi katika maisha yangu, alinifunulia kwamba, nilikuwa nimejificha nyuma ya “milango wazi ya uchungu” —matukio ya uchungu na hali za maisha yangu yaliyopita. Kupitia tena katika milango hiyo au inayofanana na hiyo, na kuwekwa huru na kuponywa kulimaanisha kukabiliana na masuala, watu, na ukweli niliyopata ukiwa mgumu, au kutowezekana kuukabili mwenyewe.

Usiogope uchungu wa uponyaji. Utajaribiwa kukwepa lakini Bwana yu karibu nawe, na anataka kukusaidia kupitia katika shida zako. Kuzipitia mara nyingi huwa bora kuliko kuzitoroka. Vumilia kinachobidi ukivumilie, ukijua kwamba kuna furaha upande ule mwingine.


Mungu haleti madhara na vidonda juu yetu. Lakini vinapoletwa juu yetu, anaweza kufanya miujiza kutoka kwa makosa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon