Moyo wenye Shukrani

Moyo wenye Shukrani

Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; nyuani mwake kwa kusifu; mshukuruni, lihimidini jina lake! —ZABURI 100:4

Mtu ambaye anatiririka ndani ya nia ya Yesu atapata mawazo yake yakiwa yamejaa sifa na shukrani. Maisha yenye nguvu hayawezi kuwepo bila shukrani. Biblia inatuagiza mara nyingi katika kanuni ya shukrani. Ni kanuni ya maisha.

Milango mingi hufunguka kwa shetani kupitia kulalamika. Watu wengine wanaugua na kuishi maisha dhaifu yasiyo na nguvu kwa sababu ya ugonjwa unaoitwa kulalamika ambao hushambulia mawaza na mazungumzo ya watu.

Tunaweza kutoa shukrani nyakati zote—katika hali zote, kwa vitu vyote—na kwa kufanya hivyo, tukaingia katika maisha ya ushindi ambayo Yesu alikufa kutupatia. Huenda ikahitaji dhabihu ya sifa na shukrani, lakini mtu ambaye anachukua muda na kutoa shukrani makusudi wakati wote huwa na furaha zaidi kuliko mtu asiyefanya hivyo.

Unaweza kuchagua kujawa na shukrani sio tu kwa Mungu lakini pia watu. Kuonyesha shukrani hubariki watu walio karibu nawe, lakini pia ni vizuri kwako kwa sababu huachilia furaha katika maisha yako.


Toa shukrani kwa Mungu, na unapofanya hivyo, utapata moyo wako ukianza kujaa uzima na nuru.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon