Yesu Alikuwa Mtimilifu kwa ajili Yako

Yesu Alikuwa Mtimilifu kwa ajili Yako

Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondololee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. 1 YOHANA 1:9 BIBLIA

Utimilifu huchochewa na ukatili wa kustahili na kufaa. Ni ile hisia sumbufu isiyoisha ya kwamba hujawahi kuwa mzuri vya kutosha. Tunafikiri vitu kama, ninafaa kuomba vizuri, kusoma Biblia zaidi, na kuwa mkarimu. Ndani yetu tunataka kumpendeza Mungu, na tuna hofu sana kwamba hatumpendezi. Hatimaye, tunaamini kwamba Mungu amesikitika nasi kwa sababu hatukufikia kiwango hicho.

Lakini njia ya kwenda kwa Mungu sio utimilifu. Watu wengine katika umati waliuliza walichohitajiwa kufanya ili wampendeze Mungu, na jibu ambalo Yesu aliwapa lilikuwa “Mwamini yeye aliyetumwa na Yeye…” (Yohana 6:29). Zaidi ya yote, Mungu anataka tumwamini na tuamini Neno lake. Unaweza kuacha kung’ang’ana kupata utimilifu na kushukuru kuwa wewe ni mwenye haki mbele za Mungu kwa sababu ya Yesu. Hauhitaji kukunua au kuchuma upendo wa Mungu. Sio wa kuuzwa—ni wa bure!


Sala ya Shukrani

Baba, nisaidie kutambua kwamba sihitaji kuchuma upendo wako au kibali. Ninakushukuru kwamba ninakubalika machoni mwako kwa sababu dhabihu ya Yesu imenipa haki yako. Nitaishi maisha yangu kukupendeza leo, sio kwa sababu nitachuma upendo wako, lakini kwa sababu ninataka kuonyesha upendo wangu kwako

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon