Mungu ananena na wewe

Mungu ananena na wewe

Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake  —Yohana 16:13

Inaonekana kama jambo kawaida na la kimsingi, lakini naamini kuna wengi ambao bado wanajiuliza kama Mungu anazungumza kweli na watu. Umewahi kujiuliza kuhusu hili? Je! Unajiuliza kama Mungu atawahi kuzungumza na wewe? Utakuwa na furaha kujua kwamba jibu ni ndiyo.

Kufikia mwisho wa wakati wake duniani, Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa.

Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake ( Yohana 16:12-13)

Yesu alipokuwa akisema maneno haya, alikuwa anaongea na watu ambao alikuwa ametumia miaka mitatu nao … bado alikuwa na zaidi ya kuwafundisha. Hii ni ya kushangaza, kwa sababu ningefikiri kwamba ikiwa Yesu alikuwa na mimi binafsi kwa miaka mitatu, mchana na usiku, ningekuwa nimejifunza kila kitu ambacho ni lazima nijue.

Lakini Yesu daima ana mengi ya kusema kwa sababu tutakuwa daima tunakabiliwa na hali mpya katika maisha ambayo anataka kutuongoza. Ndiyo maana tumepewa Roho Mtakatifu-ili tuweze kumsikia Mungu akinena, ingawa Yeye hawezi kuwa kimwili mbele yetu

Kupitia Kristo, na nguvu za Roho Mtakatifu, Mungu anataka kuzungumza na wewe ana kwa ana kwa kila siku. Anataka kukuongoza hatua kwa hatua kwa vitu vyema ambavyo amekuhifadhia.

Baba atatoa zawadi ya Roho Wake kwa wote wanaomuomba (angalia Luka 11:13). Ninataka tena kusema kwa uwazi kwamba kila mmoja wetu anaweza kusikia kutoka kwa Mungu na kuongozwa na Roho Mtakatifu kila siku. Je! Unasikiliza?


Ombi La Kuanza Siku

Mungu, naomba kuongozwa na Roho Mtakatifu. Ninaamini kwamba Wewe unaongea na mimi, na ninataka kujua ni nini unasema.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon