Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake. MHUBIRI 3:11
Tunapompokea Yesu kama Mwokozi wetu, anachukua dhambi zetu na kutupatia haki yake (tazama 2 Wakorintho 5:21). Sina hakika kwamba wengi wetu wanafahamu athari kamilifu ya jambo hilo. Bila gharama kwetu, tunafanywa wenye haki na Mungu. Huwa tunaanza kuhisi hatuna makossa badala ya kuhisi sisi ni wakosa!
Kwa nini tusichukue hatua ya imani leo na tujaribu kusema au kuwaza kitu kizuri kujihusu. Sihimizi aina mbaya ya kiburi, lakini ninakuhimiza kuwa mjasiri vya kutosha kuamini wewe ndiwe mtu wa ajabu vile Mungu alivyosema.
Katika Zaburi 139, Daudi alikiri kwamba alijua Mungu alimuumba, kisha akasema, “Matendo yako ni ya ajabu, na nafsi yangu yajua sana” (mst. 14). Daudi alishukuru kwamba aliumbwa na Mungu kwa njia ya ajabu—wewe pia! Kuwa mjasiri vya kutosha kuamini hivyo leo.
Sala ya Shukrani
Baba, nisaidie niwe na furaha ya kujua niliye ndani ya Kristo. Umeniumba kwa upekee na kuniokoa kikamilifu. Ninakushukuru kwamba mimi ni mrembo machoni mwake.