Mungu Hakukatai

Mungu Hakukatai

Baba yangu na mama yangu wameniacha bali Bwana atanikaribisha kwake. —ZABURI 27:10

Tuliumbwa ili tukubalike, sio kukataliwa. Kukataliwa ni kutupwa kama ambaye hana thamani au asiyetakikana, lakini Mungu hufanya kinyume. Anakuvuta kwake, na kukuchukua kuwa mwenye thamani sana. Ukweli kwamba Mungu alimtuma Yesu kukufia unaonyesha kwmaba unapendwa na kuthaminiwa na Mungu.

Iwapo umeng’ang’ana na masuala ya kuhusu jinsi unavyojiona katika maisha yako, huenda ikawa ni kwa sababu ya shina la kukataliwa. Uchungu wa kihisia ni mojawapo ya aina za kukatawaliwa ambao ni wa kina. Haswa kukataliwa huja kutoka kwa mtu tunayependa au kutarajia kutupenda, kama wazazi au mke au mume. Kushinda kukataliwa bila shaka si rahisi, lakini tunaweza kuushinda kupitia kwa upendo wa Yesu Kristo.

Katika Waefeso 3:18, Paulo aliliombea kanisa ili lijue kwamba “upana, urefu na uketo” wa upendo ambao Mungu alikuwa nao. Alisema hii tajriba inapita ufahamu.

Chunguza njia zote ambazo Mungu huonyesha upendo wake kwako, na utashinda kukataliwa ambako umewahi kuwa nao kutoka kwa watu wengine. Kila wakati Mungu anapokupa kibali, anakuonyesha kwamba anakupenda. Kuna nyingi ambazo yeye hukuonyesha upendo wake wakati wote. Ninakuhimiza kuanza kuchunguza siku hizo leo.


Ufunuo wa ndani wa upendo wa Mungu kwako utaharibu mzizi wowote wa kukataliwa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon