Mungu Huamuru Mamlaka

Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu na ile iliyopo imeamriwa na Mungu (Warumi 13:1) 

Nia ya heshima na unyenyekevu kwa mamlaka huhitaji kupenya katika maisha yetu ya kila siku- kwa sababu Mungu huweka mamlaka kwa usalama wetu na kukuza furaha yetu. Anatupatia mamlaka ya kiroho na ya kawaida, na ni muhimu kutii yote. Hata lazima ishara za alama zilizowekwa na watu walio mamlakani ziheshimiwe. Iwapo kuna eneo la “Hakuna maegesho,” usiegeshe hapo. Iwapo sehemu ya kuegesha tu iliyopo ni ya walemavu na wewe si mlemavu, usiegeshe hapo hata kama itamaanisha utembee masafa marefu! Taa nyekunde ikimulika, “Usitembee,” basi usitembee. Usivukie barabara popote kwa kuwa tu una haraka. Iwapo uko katika sehemu ya “Hakuna kupita,” katika barabara kuu, basi usipite.

Huenda ukawa unafikiria, hata hivyo vitu haviwezi vikaleta tofauti yoyote. Hayo ni mambo madogo, nina matatizo makubwa yanayohitaji majibu. Sisi wote tutaendelea kuwa na matatizo yetu makubwa hadi tutakapojifunza kwamba, uteuzi wetu wa mambo madogo kama kuheshimu mamlaka au kutoheshimu una athari kubwa sana kwa maisha yetu.

Tabia kama hizo nimeeleza huakisi nia ya ukaidi kwa mamlaka, na hilo huzuia uwezekano wetu wa kusikia sauti ya Mungu kwa sababu Mungu mwenyewe huweka mamlaka katika maisha yetu na hutaka tuyatii. Tunamheshimu tunapoheshimu mamlaka inayotuzingira.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Kuwa mwangalifu kumtii Mungu katika vitu vidogo na vitaleta tofauti kubwa katika maisha yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon