Mungu Hubadilisha Watu Kupitia Kwa Maombi

Mungu Hubadilisha Watu Kupitia kwa Maombi

Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote. —1 Timotheo 2:1

Katika Kutoka 32, Musa aliwaombea wana wa Israeli ili hasira ya Mungu isiwaangamize. Ni mfano unaosisimua ambao unatoa picha ya jinsi maombi yanayofanywa kwa uaminifu yanaweza kubadilisha hali.

Kuna nyakati ambazo huwa najikuta nikiongozwa kuomba ili Mungu amwonee huruma mtu, au kuendelea kufanya kazi nao na kufanya mabadiliko yanayohitajika ndani yao.

Kama Yesu alivyowaambia wafuasi wake Gethsemane, tunaweza “kukesha na kuomba” (Mathayo 26:41). Tuna nafasi ya kuombeana, sio kuhukumiana na kudondoana makosa. Mungu huturuhusu kutambua mahitaji ya watu ili tukawe sehemu mojawapo ya majibu yao, na siyo sehemu mojawapo ya matatizo yao. Kumbuka sisi si wafinyanzi. Mungu ndiye, na bila shaka hatujui jinsi ya “kuwafinyanga” watu. Hatuwezi kuwabadilisha watu, lakini tunaweza kuomba na kumtazama akifanya kazi.

Watu wanapodhurika, hata kutokana na uteuzi wao mbaya, mara nyingi huwa wanaupofukia ukweli. Tunaweza kuwombea ili macho yao yafunguke na kwamba waone ukweli ili uwaweke huru. Watu wanaodhurika huhitaji Mungu kuingilia kati, katika maisha yao, lakini wasipojua kuliitia jina lake, tunaweza kusimama katika pengo, kati yao na Mungu kama waombezi na kuona upenyo hata tunapoendelea kuomba.


Tunaweza kufanya maombi na tumwache Mungu afanye kazi hiyo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon