Mwenye shukrani kwa Neema

Mwenye shukrani kwa Neema

Na Stefano, akijaa neema na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu. MATENDO YA MITUME 6:8 BIBLIA

Neema inaweza kuwa ya manufaa kwako katika maisha yako ya kila siku. Kwa mfano: ukiingia katika hali ambayo inaanza kukufanya ukate tamaa, simama tu na useme, “Ee, Bwana nipe neema.” Halafu uamini kwa imani kwamba Mungu amesikia maombi yako, na ushukuru kwamba anashughulikia hali hiyo unapoendelea na shughuli zako za kila siku.

Imani ndiyo njia ambayo wewe na mimi hupokea neema ya Mungu ili kutimiza mahitaji yetu. Biblia inasema kwamba neema ni nguvu za Mungu ambazo huja kwetu kupitia kwa imani yetu ili kutimiza mahitaji yetu. Utakapoanza kuhisi kukata tamaa wakati ujao, tulia na uhiari kutegemea neema ya Bwana.


Sala ya Shukrani

Baba, ninakushukuru kwa nguvu za neema yako katika maisha yangu. Nisaidie kukutegemea leo na sio kwa nguvu zangu mwenyewe. Ninakushukuru kuwa uko nami na ninaweza kuweka imani yangu ndani yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon