Na je..?

Na je..?

Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; Wafilipi 3:13

 Na je …? Kwa muda mrefu mtu anaishi, huenda anajiuliza na je…? na kujisikia huzuni au majuto yanayosababisha mara nyingi. Habari njema ni kwamba kwa mfuasi yeyote wa Yesu, “na je?” haipaswi kuwa na majuto juu ya siku za nyuma lakini changamoto ya kusisimua ya kuona wakati ujao Mungu anao kwao.

Najua ya kutaniko ambalo lilikuwa likipewa changamoto na mchungaji wao kufanya mambo manne rahisi (kwa mwezi tu) ili kujitakasa kwa mwaka ujao. Aliwaomba kuomba kila siku, kufunga siku moja kwa wiki, kutoa fungu la kumi, na kuleta mtu ambaye hajaokoka kila wiki  kanisani. Matokeo yake yalikuwa mafanikio yasiyotarajiwa katika maisha ya kanisa hili. Uwepo wa Mungu ukawa na nguvu katika huduma. Ufanisi wa kifedha ulikuja kwa miradi ya huduma na majengo yaliyopendekezwa. La kusisimua zaidi kwa wote, wanachama wa kanisa waliingia msimu wa ajabu wa kuleta nafsi waliopotea katika ufalme wa Mungu.

Ninataka kukupa changamoto: Je, ikiwa utamfuata Mungu leo, kama kanisa hilo? Na je, ikiwa ukijitolea maisha yako kabisa kwa Yeye? Na je, ikiwa  wewe utajisukuma mbele, tayari kuona nini Mungu anaweza kufanya? Nini kinaweza kutokea?

OMBI LA KUANZA SIKU

Bwana, sitaki kutumia maisha yangu kuuliza “na je?” bila kuona mafanikio yoyote katika maisha yangu. Ninafanya ahadi mpya ya kukufuatilia leo, nimefurahi kuona mambo ya ajabu utakayotenda katika maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon