Ndiyo na La

Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye mwanawe akimwomba mkate atampa jiwe? Au akiomba samaki atampa nyoka? (MATHAYO 7:9-10)

Sisi huwa si werevu wa kutosha kila mara kujua vitu sawa vya kuomba, lakini andiko la leo linatuahidi ya kwamba, tukiomba mkate, Mungu hatatupatia jiwe, na tukiomba samaki, hatatupa nyoka. Kuna wakati ambao huwa tunafikiri tunaomba mkate, na kumbe kwa kweli tunaomba jiwe. Kwa maneno mengine, tunaweza kuwa tunaomba kitu ambacho kwa kweli tunaamini ni sawa, lakini Mungu anajua kujibu maombi hayo ni kitu kibaya sana ambacho atawahi kufanya.

Tuna uwezo, kwa kutokujua, kuomba kitu hatari au kibaya kwetu bila kutambua. Katika haili kama hiyo, tunahitaji kufurahi kwamba Mungu huwa hatupi! Katika hali kama hizo, hatukujua kabisa kwamba Mungu angesema “ndiyo” kwa ombi hilo ingekuwa kama kuruhusu nyoka aingie nyumbani mwetu. Lazima tumwamini kiasi cha kusema, “Mungu, nina ujasiri wa kukuomba chochote. Lakini sitaki chochote ambacho si cha mapenzi yako juu ya maisha yangu. Na ninakuamini, Mungu. Nisipokipata, nitajua kwamba wakati haujafika au kwamba una kitu bora zaidi kwa ajili yangu na sijafikiria tu kukuomba bado.” Usiwahi kuwa na fikra mbaya kwamba Mungu huwa hakupi kila kitu unachotaka.

Mungu anataka tubarikiwe. Mbali na kutaka tuwe na kile tunachotaka, anataka kiwe kizuri sana pia. Iwapo kweli tunamwamini Mungu, lazima tumwamini anaposema “la” kwa maombi yetu jinsi tu tunavyomwamini akisema “ndiyo” kwa maombi hayo.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Mwamini Mungu anaposema “la” na anaposema “ndiyo.”  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon