Neema yake Itakupitisha

Neema yake Itakupitisha

Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia… — 1 PETERO 4:14

Je, umeteseka kwa kuwa Mkristo? Ukafanyiwa mizaha, ukapuuzwa, ukakosa kueleweka, ukakosa kupewa madaraka au kufanyiwa jambo lolote baya zaidi?

Wengine wanafikiri ni jambo baya sana kuteswa kwa sababu ni Wakristo, lakini Mungu huliona kwa mtazamo tofauti kabisa. Mungu huwa hatarajii tuteseke kwa ajili yake bila usaidizi wake. Tunaweza kuamini bila kuyumbayumba kwamba wakati wowote tunapoteswa kwa njia yoyote kwa sababu ya imani yetu ndani ya Kristo, Mungu anatupatia kipimo zaidi cha neema ili kikabiliane na mashambulizi. Kuna nguvu za kushinda!

Tunapotambua na kutegemea uwepo wa Mungu katika maisha yetu, tunaweza kupitia katika hali ngumu na bado tuwe wenye furaha na amani. Kama vile Shadraka, Meshaki na Abdnego katika Danieli 3:21-27, tunaweza kwenda katika tanuri la moto au katika mateso na kung’ang’ana, na kutoka hata bila harufu ya moshi.

Tukibaki imara, huku tukimtumainia Mungu kwa ujasiri katika nyakati ngumu, tunaweza kuhakikishiwa kwamba utukufu wa Mungu utakuwa thawabu yetu.


Karibisha uwepo wa Mungu katika maisha yako na ufurahie kwa ajili ya neema utakayoona ikikuwezesha kwa chochote ambacho huenda unakabiliana nacho.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon