Nguvu ya Kiroho

Mmoja angefukuzaje watu elfu, wawili wangekimbizaje elfu kumi, kama mwamba wao asingaliwauza, kama Bwana asingaliwatoa? (Kumbukumbu la Torati) 

Kama nilivyosema, Mungu hujibu maombi ya makubaliano kama watu wanaoomba wanaonyesha makubaliano tayari katika maisha yao ya kila siku. Hufurahia wanaolipa gharama ya kuishi katika makubaliano, umoja na upatanifu kiasi cha kuwaambia kwamba, “Mnapokubaliana hivyo, nguvu zangu huachiliwa kati yenu. Nguvu za makubaliano yenu ni nyingi sana mtapata mpenyo- hakuna shaka kuhusu hilo. Nitajibu.”

Unaona, makubaliano ni yenye nguvu kiasi kwamba ni kanuni ya kuzidisha, sio kuongeza. Ndiyo kwa sababu andiko la leo linasema kwamba mtu mmoja angefukuzaje elfu na wawili wangekimbizaje elfu kumi. Lakini umoja huamrisha baraka za Mungu- na baraka za Mungu huzidisha. Kwa sababu hiyo, ombi la makubaliano ya kweli yana nguvu katika ulimwengu wa kiroho.

Tunapogawanyika, tunakuwa wadhaifu na tunapoungana, tunakuwa na nguvu. Kwa hakika nguvu zilizopo kwa ajili yetu ni zaidi ya bidii tunazotumia kudumisha umoja na upatanifu. Haijalishi kile atakachofanya mtu mwingine au kukosa kukifanya, wewe fanya sehemu yako na Mungu atakubariki.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Huwezi kufanya ukaelewana na kila mtu, lakini unaweza kukataa kukasirishwa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon