Sala ya Yesu Kwako

Sala ya Yesu Kwako

Na sasa naja kwako na maneno haya nayasema ulimwenguni ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao. YOHANA 17:13

Yesu alimwomba Baba yake katika Yohana 17:13, Aliomba kwamba tuwe na furaha. Alisema, “Ninayasema maneno haya ili furaha yangu iwe tele, ikamilike na kutimilika ndani yao…” Ikiwa Yesu mwenyewe anasema na kuomba maneno yenye nguvu hivyo kuhusu matamanio yake kwetu sisi kuwa na furaha, tutashuku vipi kwamba Mungu anataka tuwe na furaha na tufurahie maisha yetu?

Iwapo ni matamanio ya Mungu kwamba tufurahie maisha, basi kwa nini watu wengi wana dhiki na hawana furaha? Pengine ni kwa sababu sisi hushindwa kuweka nia zetu kwa kufurahia maisha. Tunaweza kujipata katika mkondo wa kuishi kwa kuvumilia badala ya kufurahia. Lakini nia mpya itakuachilia kuanza kufurahia maisha kwa njia ambayo hujawahi kuyafurahia. Kadri unavyofurahia maisha, ndivyo itakavyofurahisha kuwa karibu nawe, kwa hivyo anza leo na usichelewe.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru, Baba, kwamba ni mapenzi yako kwangu mimi kuwa na furaha. Haijalishi hali zinavyoonekana karibu nami, nitachagua kuishi aina ya maisha uliyo nayo kwa ajili yangu. Asante kwa kuwa ninaweza kuwa na furaha tele na nyingi kila siku ya maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon