Shina la Uchungu

Shina la Uchungu

Mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo… —WAEBRANIA 12:15

Tunaporuhusu kutokusamehe katika maisha yetu, tunajawa na uchungu. Uchungu unarejelea kitu ambacho kina ladha kali.

Tunakumbuka kwamba wana wa Israeli walipokuwa karibu kuongozwa kutoka Israeli, waliambiwa na Bwana kutayarisha chakula cha pasaka kilichojumlisha mimea chungu. Kwa nini? Mungu alitaka wale hiyo mimea chungu kama kumbukumbu ya uchungu wa maisha waliopitia utumwani.

Uchungu huanza vipi? Unakua kutoka kwa mzizi, ambao tafsiri ya King James inazungumzia kama mzizi wa uchungu. Mzizi wa uchungu kutoka kwa mbegu ya kutokusamehe huzaa matunda ya uchungu.

Uchungu hutokana na makosa tuliyotendewa ambayo huwa hatusamehei, mambo tunayofikiriafikiria hadi tunayafanya kuwa makubwa kuliko inavyostahili. Kadri tunavyoyaruhusu kukua na kutukera, ndivyo mizizi yake inazidi kukita. Jifunze kuwa mwepesi wa kutubu kwa sababu ukifanya hivyo haraka, itakuwa rahisi!


Mzizi wa uchungu utaambukiza nafsi yetu yote— nia na tabia, mtazamo, na mahusiano yetu, hususan uhusiano wetu na Mungu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon