Shukrani kwa Amani

Shukrani kwa Amani

Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani. WAKOLOSAI 3:15

Amani ni urithi wetu kutoka kwa Yesu, na hiki ni kitu cha kushukuru kwacho. Biblia inafundisha kwamba amani ndiyo itakayokuwa “mwamuzi” katika maisha yetu, ikileta suluhisho kwa kila jambo linalohitaji kufanyiwa uamuzi. Ili kupata na kudumisha amani katika mioyo yetu, lazima tuchague kufuata mwongozo wa Roho Mtakatifu na kujifunza kusema hapana kwa vitu vingine. Kwa mfano, tusipohisi kuwa na amani kuhusu kitu, tusiwahi kukifanya. Na kama hatuna amani kama tunafanya kitu, basi tusitarajie kuwa na amani baada ya kukifanya.

Uwepo wa amani unaweza kutusaidia kuamua na kutatua kikamilifu maswali yote yanayotokea katika mawazo yetu. Ukiacha Neno la Mungu liwe na makao katika moyo wako na mawazo yako, litakupa ufahamu, hekima na amani.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru leo, Baba, kwamba umenipa amani kama urithi wangu. Nisaidie kuacha kila wasiwasi na mfadhaiko ambao utajaribu kunishusha. Badala yake, ninachagua kuruhusu amani iniongoze katika vitu vyote maishani mwangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon