Siko Peke Yangu

Na Yesu hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani akajaribiwa na Ibilisi… (LUKA 4:1-2)

Tunajifunza kutokana na maandiko ya leo kwamba punde tu Yesu alipobatizwa katika Roho Mtakatifu, aliongozwa kwenda nyikani na Roho Mtakatifu, kujaribiwa na Ibilisi kwa muda wa siku arobaini usiku na mchana. Bila shaka hiyo ilikuwa tajriba ngumu, lakini Yesu akatii uongozi wa Roho. Alimtumaini Roho Mtakatifu, akijua kwamba magumu aliyokuwa akikabiliana nayo yangegeuka na kuwa mema kwa ajili yake mwishowe.

Mwishoni mwa hizo siku arobaini nyikani, Yesu alianza huduma yake ya umma, tunavyoona katika Luka 4:14: “Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando.” Ilimlazimu Yesu kuhiari kufuata uongozi wa Roho Mtakatifu hadi kwenye uwezo na umashuhuri; Alikuwa pia ahiari kumfuata kwenye nyakati ngumu, nyakati za majaribu na kujaribiwa.

Kutii Mungu katika nyakati ngumu husaidia kukuza tabia za kiungu. Yesu alitupatia mfano ambao tunafaa kufuata. Kufuata uongozi wa Roho Mtakatifu wakati wa misimu ya matatizo hukuza imani, udhamirifu, na nguvu ndani yetu- sifa ambazo Mungu anataka tuwe nazo.

Mungu ametupatia Roho Mtakatifu ili atusaidie kutimiza mipango yake juu ya maisha yetu. Wakati mwingine, lazima tukabiliane na matatizo ili kukuza tabia tunazohitaji ili kufanya kile Mungu amepanga. Lazima tukumbuke kila wakati kwamba huwa hatukabiliani na chochote- matatizo au nyakati nzuri-tukiwa peke yetu. Roho Mtakatifu huwa nasi kila wakati kutusaidia na njia zake huwa nzuri kabisa kila wakati.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Usiogope nyakati ngumu, kwa sababu hukutia nguvu hatimaye.   

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon