Tarajia Kitu Kizuri

Tarajia Kitu Kizuri

Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu. WARUMI 15:13

Mojawapo ya msukumo wenye nguvu sana ulimwenguni ni tumaini. Na kama mtoto wa Mungu, unaweza kuwa na tumaini lisilo na kikomo. Hicho ni kitu cha kumshukuria Mungu!

Tumaini ni matarajio ya furaha kwamba kitu kitafanyika katika maisha yako. Ni kutarajia kitu kizuri. Unatarajia nini? Umewahi hata kufikiria kuhusu hilo? Iwapo hutarajii chochote, au kama unatarajia tu machache, utapata unachotarajia.

Kila wakati huwa ninasema, “afadhali nitumainie kitu kikamilifu na nipate nusu yake kuliko kutumainia kitu nusu na nipate kikamilifu.”

Mungu anataka umtumainie na utarajie kitu kizuri kwa furaha. Iwapo uko katika hali ngumu, tarajia kwamba itabadilika. Iwapo uko katika hali nzuri leo, tarajia kuwa itakuwa hata nzuri zaidi. Mungu ni Mungu wa tumaini.


Sala ya Shukrani

Bwana, asante kwa nguvu za tumaini katika maisha yangu. Asante kwamba unaenda kufanya kitu kizuri, na ninaweza kukuamini na kutumainia mema.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon