Tumaini Jipya kwa Kila Siku

Ni huruma za Bwana kwamba hatuangamii, kwa kuwa rehema zake hazikomi. Ni mpya kila siku asubuhi; uaminifu wako ni mkuu. —MAOMBOLEZO 3:22–23

Ninapenda vile Mungu amegawanya mchana na usiku. Haijalishi vile siku fulani ilivyo ngumu au yenye changamoto, macheo huleta tumaini jipya. Mungu hututaka kuweka ya kale nyuma yetu kila mara na kupata mahali pa “mianzo mipya.”

Pengine umehisi kufungiwa katika dhambi fulani au uraibu, na ingawa umetubu, bado unahisi kuhukumika. Iwapo hivyo ndivyo ilivyo, hakikishiwa kwamba toba ya kweli huleta mwanzo mpya wa kupendeza kwa sababu ya ahadi ya Bwana ya msamaha.

Ni wakati ule tu ambao unaelewa huruma mkuu wa Mungu na kuanza kuupokea ndipo utaelekea kuwaonyesha wengine huruma. Huenda ukawa unadhurika kutokana na jeraha la kihisia. Njia ya kusahau yaliyopita na kusamehe mtu aliyekukosea. Unajisaidia unaposamehe.

Mungu ana mipango mipya katika upeo wa maisha yako, na unaweza kuanza kuitambua kwa kuchagua kuishi katika wakati uliopo na sio kwa yaliyopita. Kufikiria na kuzungumza kuhusu ya kale hukufunga ndani yake. Achilia yaliyofanyika jana, fanya uamuzi wa kupokea upendo wa Mungu na msamaha leo, ili ufurahie kuhusu mpango wake wa kesho.


Huruma wa Mungu ni mpya kila asubuhi.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon