Tunda lililo Moyoni Mwako

Tunda lililo Moyoni Mwako

Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. —MATHAYO 7:18

Wakati wa miaka yangu michache ya kwanza ya huduma, nilitumia muda wangu mwingi wa maombi nikimwomba Mungu anipe vipawa vyenye nguvu na uwezo ambavyo vingenisaidia kuwa mhubiri mwenye mafanikio. Nililenga kwenye vipawa nilivyohitaji, lakini sikufikiria sana kuhusu tunda la Roho. Lazima nikubali kuwa nilijali sana kuhusu nguvu kuliko hulka ya kiungu.

Halafu siku moja, Bwana akaninenea, “Joyce, iwapo ungeweka tu nguvu na wakati hata nusu katika kuomba kuhusu na kujaribu kukuza tunda la Roho vile ulivyo na vipawa, tayari ungekuwa na vyote.”

Kama Wakristo, wengi wetu huomba kwamba Mungu atatupatia nguvu kuu ya Roho, lakini umuhimu wetu wa kwanza kwa kweli unafaa kuwa kukuza tunda la Roho—upendo, furaha, amani, huruma, wema, upole na ujidhibiti. Kadri tunavyomkaribia Mungu, ndivyo tutakavyozalisha matunda kikawaida.

Tunajulikana kwa matunda yetu, sio kwa vipawa vyetu. Watu wakiona tunda la Roho wa Mungu katika maisha yako, wanaona kile Mungu anafanya katika maisha yako. Leo ninawahimiza kumwomba Mungu kupalilia tunda la Roho Mtakatifu katika maisha yako kila siku. Iwapo utalenga tunda, nguvu zitafuata.


Watu hutaka kuona iwapo kile ulicho nacho ni cha kweli kabla ya kusikiliza unachosema.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon