Una uwezo

Una uwezo

Yesu akawatazama, akawaambia “Kwa binadamu haiwezekani, lakini kwa Mungu si hivyo, maana kwa Mungu mambo yote huwezekana” Marko 10:27

 Ni jambo la kushangaza jinsi watu walivyo na uwezo wa kutenda mengi lakini hawafanyi lolote.Hawachukui hatua kutoka na kutumia vipawa ambavyo Mungu amewapa kwa sababu wao hata hawaamini kwamba Mungu amewapa vipawa hivyo. Je, wewe ni mmoja wao?

Ukweli ni kwamba Mungu ametupa kila mmoja vipawa, karama na ujuzi. Ana mpango wa ajabu juu yako na amekupa uwezo wa kutenda mambo makuu katika ufalme wake. Lakini usipojiona jinsi Yeye anavyokuona na kumwamini kukuwezesha kutumia vipawa vyako, kamwe hutafikia kilele cha kile angependa ufanye.

Ikiwa unajiona duni, usiye wa maana na bila ujuzi wowote, ningependa kukuambia kwamba Mungu amekuumba na kukupa uwezo wa ajabu sana. Na ikiwa utamwamini Mungu na kukubali kwamba unaweza kutenda kile anataka utende, basi utatimiza hatima yake juu ya maisha yako.

Kumbuka kwamba mambo yote yanawezekana na Mungu. Unapoweka tumaini lako kwake, basi utaweza kuishi kutimiza wajibu wako kama Mkristo.

 OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, nisaidie kujiona kama unavyoniona, nione vipawa na talanta ulizonipa. Naamini uliniumba na uwezo wa ajabu kwa sababu Wewe ni Mungu mkuu.Siku ya leo, nalieka tumaini langu kwamba nikiamini kwmba kwako, mambo yote yanawezekana.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon