Unafikiria Nini Kujihusu?

Unafikiria Nini Kujihusu?

Kisha huko tuliwaona wanefili [majitu], wana wa Anaki, waliotoka kwa hao wanefili, tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi. —HESABU 13:33

Tunasoma katika Hesabu kuhusu vile Musa aliwatuma wanaume kumi na wawili kutalii Nchi ya Ahadi ili kuona iwapo ilikuwa nzuri au mbaya. Wanaume kumi miongoni mwao wakarudi na kile ambacho Biblia inasema “ripoti ovu” (Hesabu 13:32). Walimwambia Musa, “Ile nchi ni nzuri, lakini ina majitu ndani yake!” Pia walijiita “mapanzi,” kumaanisha waliamini hawakuwa na maana na wasingeweza kumshinda adui.

Hofu waliyokuwa nayo dhidi ya majitu iliwazuia watu wa Mungu kuingia katika nchi aliyokuwa aliyokuwa ameahidi atawapa. Kwa kweli si majitu yaliyowashinda watu hawa; ilikuwa picha yao mbaya kujihusu. Waliona tu majitu; walikosa kumwona Mungu, na wakashindwa kuamini kwamba wakiwa na Mungu, wangeweza kufanya mambo yote waliyohitaji kufanya.

Ni Yoshua na Kalebu peke yao ndio walikuwa na fikra sawa. Kalebu akawatuliza watu mbele ya Musa akasema, “Na tupande mara, tukaitamalaki; maana twaweza kushinda bila shaka.” (Hesabu 13:30). Walikuwa na fikra kwamba Mungu alitaka wawe nayo. Waliamini kwamba wakiwa na Mungu mambo yote yaliwezekana.

Mungu alikuwa na mustakabali wa utukufu aliokuwa amewapangia Waisraeli wote, vile tu anavyotufanyia sisi, lakini ni wale tu walio na fikra zinazostahili juu ya Mungu na kujihusu ndio wataishi katika mpango huo na kuufurahia.


Mungu hana fikra mbaya juu yako, usiwe na moja kujihusu!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon