Kudhihirisha Upendo wa Mungu Usio na Masharti

Kudhihirisha Upendo wa Mungu Usio na Masharti

Kuchukiana huondokesha fitina bali kupendana husitiri makosa yote. MITHALI 10:12

Shukuru kwamba, Mungu hatuhitaji kuchuma upendo wake, na hatufai kuwahitaji wengine kuchuma wetu. Tunafaa kutambua kwamba upendo ni kitu ambacho tunafaa kuwa, sicho kitu tunachofanya halafu tena tusikifanye. Hatuwezi kukiwasha na kukizima, kutegemea tunayetaka kumpa na vile wanavyotuchukulia.

Wakati mwingine tunaomba tuweze kuwapenda wasiopendeka, halafu tunajaribu tuwezavyo kuepuka kila mtu asiyependeka ambaye Mungu anatutumia. Watu wengine hutumwa maishani mwetu kwa kusudi la pekee la kutupiga msasa. Sio tu watu wengine walio na kingo zinazokwaruza, sisi pia tunazo. Kujifunza kutembea katika upendo na watu wasiopendeka ni kifaa muhimu ambacho Mungu hutumia kujenga ukomavu wetu wa kiroho.

Amini usiamini, tunafaa kushukuru kwa watu wote wasiopendeka walio katika maisha yetu kwa sababu wanatusaidia: wanatunoa na kutusafisha kwa matumizi ya Mungu.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwa nafasi ya kupenda watu kwa njia hiyo sawa isiyo na masharti ambayo unanipenda. Nisaidie kumpenda kila mtu—hata wale ambao ni wagumu kutangamana nao. Ninakushukuru kuwa unawatumia kuninoa na kunisafisha kwa matumizi yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon