Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana, maana pasipo mimi [mkikatwa kutoka umoja nami] ninyi hamwezi kufanya neno lolote. —Yohana Mtakatifu 15:5
Nilikuwa mtu wa kujitegemea sana, na Mungu akaanza kunizungumzia Yohana 15:5 mapema katika kutembea kwangu naye. Tunapokuja katika nguvu za Mungu, tunaanza kumtegemea kikamilifu. Imani inahusisha kumtegemea Mungu kabisa, kuamini nguvu zake, hekima na wema.
Tunahitajika kumwegemea na kumtegemea Mungu, huku tukijiondoa nira zote na kuziweka juu yake. Bila usaidizi wa Mungu, hatuwezi kubadilisha chochote katika maisha yetu. Hatuwezi kujibadilisha, kubadilisha waume au wake zetu, familia zetu, marafiki zetu, au hali zetu. Kwa kweli pasipo yeye, hatuwezi kufanya lolote.
Tunasusia amani na furaha na kukosa kuacha Mungu awe Mungu. Huwa tunajaribu kufikiria kuhusu vitu ambavyo hatufai hata kugusa na nia zetu. Hakuna kitu kigumu wala cha ajabu kwa Mungu, lakini vitu vingi ni vigumu sana kwetu. Kwa usaidizi na uongozi wa Roho Mtakatifu, tunaweza kukua tukafikia mahali ambapo tutapumzika katika ukweli kwamba tunamjua anayejua majibu yote, hata kama hatujui… na tunaweza kumwamini!
Inaweka huru kusema, “Bwana, sijui la kufanya, na hata kama ningejua, nisingefanya. Lakini macho yangu yako juu yako. Nitangoja na nikutazame ukinitendea.”