Uteuzi Ni Wako

Uteuzi ni Wako

Maana sisi ni kazi ya Mungu, tuliumbwa katika Kristo Yesu, [tumezaliwa upya] tutende matendo mema [yaliyopangwa mapema], ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo [tuishi maisha mema aliyotupangia na kuyatayarisha ili tuyaishi]. —Waefeso 2:10

Mungu amekupa zawadi ya ajabu: uteuzi huru. Mungu anakupa nafasi ya kujikubali vile alivyokuumba kuwa, lakini una uteuzi huru na unaweza kukataa kufanya hivyo kwa uteuzi wako. Kukubali kunamaanisha kukiona kama cha kawaida, kinachofaa au kilicho sawa.

Watu wanaojikataa hufanya hivyo kwa sababu huwa hawawezi kujiona kama wanaofaa au walio sawa. Wao huona tu kasoro zao na udhaifu, sio urembo wao na nguvu. Hizi ni fikra zisizo sawa, ambazo hutiwa na watu maarufu wa zamani ambao waliona yaliyokuwa dhaifu na mabaya badala ya nguvu na mazuri.

Katika Amosi 3:3, tunasoma, “Je, watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?” Unaweza kutembea na Mungu—unaweza kuwa karibu naye—ukiamua kupatana naye. Anasema anakupenda na kukukubali; kwa hivyo, ukipatana naye, huhitaji tena kujichukia au kujikataa.


Mungu alipokuumba, aliumba kitu cha ajabu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon